







| Taarifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu kwa mnasaba wa kuaga dunia Allamah Fadhlullah |
|
|
|
| Written by Baraza |
| Monday, 05 July 2010 12:02 |
|
Kwa mnasaba wa kuaga dunia na kurejea kwa Mola Muumba Ayatullah Muhammad Hussein Fadhlullah, Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu imetoa taarifa na salamu za rambimbi kwa Waislamu wote. Matini ya taarifa hiyo ni hii ifuatayo: Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea sote. Kwa huzuni na masikitiko makubwa tumepokea habari ya kuaga dunia rijali wa elimu na jihadi, hatibu hodari, marjaa na mwanafikra mkubwa wa Kiislamu Ayatullah Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. Alikuwa mstari wa mbele katika jihadi, ikhlasi na kuhudimia dini tukufu na umma wa Kiislamu na alijisabilia kwa ikhlasi kwa ajili ya kupandisha juu neno la haki, kulinda umoja wa Waislamu na kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu. Hakika umma wa Kiislamu umempoteza mujtahidi aliyekuwa na fikra mpya, mwanamageuzi mkubwa, mtu aliyepigania umoja, mhakiki hodari wa masuala ya Qur'ani, kiongozi shupavu wa kisiasa, mwanafikra aliyeacha athari nyingi katika nyanya mbalimbali, mlinganiaji mkweli aliyeingia katika mbuza zote kwa nia ya kuwasilisha sauti ya haki na mwanajihadi mkubwa aliyesimama kidete na imara mbele ya ubeberu wa kimataifa wa Wazayuni na njama za maadui wa Uislamu. Kutokana na kifo cha mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu mbaye daima alikuwa akitetea na kuunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika nyanja zote, Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu inatoa mkono wa pole kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, marajii taklidi, vyuo vikuu vya kidini, wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu, watetezi wote wa umoja wa umma wa Kiislamu, familia ya marehemu na wananchi wa Lebanon. Jumuiya hii pia inamuombea marehemu Ayatullah Fadhlullah maghufira ya Mwenyezi Mungu na darja za juu pepo.
|
| Last Updated on Monday, 05 July 2010 12:14 |
Design by Andishe Velayat