







| Shekhe Mkuu wa Al Azhar apinga ombi dhidi ya Mashia |
|
|
|
| Sunday, 20 June 2010 04:21 |
|
Kwa mujibu wa kanali ya Al Alam, Sheikh Saad bin Hamdan Al-Ghamdi wa Chuo Kikuu cha Umm al-Qura nchini Saudi Arabia hivi karibuni alimkosoa vikali Shekhe Mkuu wa Al Azhar kutokana na misimamo yake ya kuyakubali Madhehebu ya Kiislamu ya Shia Ithnaashari. Alimtaka akanushe uungaji mkono wake kwa Mashia na asiwatambue rasmi. Hatahivyo Ahmed Mohammad El-Tayyib, Shekhe Mkuu wa Al Azhar katika mahojiano na gazeti la Al Watan la Kuwait amesema Mashia na Masunni ni mabawa mawili ya Umma wa Kiislamu. Ameongeza kuwa katika historia ya miaka 1400 ya Uislamu, madhehebu haya mawili hayajapigana. Amesisitiza kuwa mivutano inayoshuhudiwa leo inatokana na fitina zinzozushwa baina ya Waislamu ili kuibua mapigano ya kimadhehebu. Shekhe Mkuu wa Al Azhar amesema kuyakurubisha madhehebu ya Kiislamu kutakuwa kati ya masuala muhimu zaidi ya Chuo Kikuu cha al Azhar katika siku za usoni. Amesema hitilafu baina ya Shia na Sunni ni katika masuala ya pembeni na kwamba wote wanakubaliana kuhusu misingi ya Uislamu. Sheikh Ahmed El-Tayyib amesema Al Azhar inakaribisha wanafunzi Mashia kutoka Iran na maeneo mengine duniani. |
| Last Updated on Sunday, 20 June 2010 04:30 |
Design by Andishe Velayat